TUTAMSAIDIA RAIS SAMIA KWA UAMINIFU NA WELEDI WOTE-MAJALIWA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wasaidizi wote wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wamejipanga kuhakikisha kwamba wanamsaidia kwa weledi wote, uaminifu ili malengo na matamanio yake ya kuwaletea Watanzania maendeleo yaweze kufanikiwa. Hivyo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwa na imani ya Serikali kwa sababu imedhamiria kuwatumikia kwa lengo la